Vitu Muhimu Vya Kufahamu Kuhusu Bodaboda za Kuchaji
Bodaboda ya kuchaji na umeme ni nini?
Ni pikipiki inayotumia betri ya kuchaji na umeme na inayotumia mota kuzungusha tairi badala ya injini.
Je nini faida za kutumia bodaboda ya kuchaji?
Faida zake ni hizi: haitumii mafuta, huhitaji kubadilisha oil na haina kelele wala haitoi moshi hivyo ni rafiki kwa mazingira.
Je pikipiki ya kuchaji ina spidi hadi ngapi?
Spidi yake ni 80km/kwa saa
Je pikipiki ya kuchaji inaweza kwenda umbali gani hadi chaji kuisha?
Inatembea umbali wa km150-200
Je vipi kuhusu upatikanaji wa spea kama mota, betri, swichi ya gia na dashbodi endepo vikiharibika?
Spea hizi zote zinapatikana hapa katika ofisi ya kampuni ya Techno Roads Eye
Je bodaboda ya kuchaji inaweza kubeba mzigo?
Ndiyo inaweza kubeba mzigo unaolingana na uzito wa mtu.
Je Betri inakaa muda gani hadi kuisha?
Betri inakaa hadi muda wa masaa 8.
Inachukua muda gani Betri kujaa inapochajiwa?
Inachukua muda wa masaa 2.
Inachukua muda gani Betri kujaa inapochajiwa?
- Vitu muhimu kuzingatia ili betri iweze kudumu ni:
Chaji betri kwa masaa 6 hadi 9 kwa mara ya kwanza unaponunua pikipiki - Hakikisha betri inachajiwa na kujaa hadi asilimia 100%.
- Usisubiri betri kuisha kabisa hadi asilimia 0%, chaji mara inapokaribia asilimia 20%
- Usijaribu kubusti betri kwa kutumia waya, utasababisha shoti na kuua betri
- Usijaribu kuingiza betri kwenye maji
Hifadhi betri mahali pa ukavu - Usiweke betri mahali penye joto kali zaidi ya nyuzi 60
- Tumia tu chaja uliyopewa wakati wa kununua pikipiki kwa ajili ya kuchajia
- Usiachebetri bilakuchaji kwa muda mrefu, lazima kama haitumiki ichajiwe angalau mara moja katika mwezi
- Ukiona dalili za hitilafu ya betri kama vile kutoa harufu isiyo ya kawaida, kutoa joto kali, rangi kubadilika au hitilafu yoyote; tafadhali sitisha kutumia hiyo betri na wasiliana na fundi kwa ajili ya matengenezo.